Kanisa Anglikana Mtaa wa Mt. Mikaeli na Malaika wote Mtwara kwa sasa lipo katika shughuli za upanuzi wa Kanisa hilo ili kuongeza ukubwa wa kanisa hilo pamoja na ofisi za wachungaji wake pia ukumbi wa mikutano utakaongezwa katika sehemu inayopanuliwa. Upanuzi huu unatarajia kugharimu pesa inayotarajiwa kufikia
Tsh 500,000,000/= Pesa hii kwa kiasi kikubwa inatarajiwa kupatika kutoka kwa Wakristo wa Kanisa hilo kupitia michango mbalimbali pia kupitia michango kutoka kwa viongozi mbalimbali na marafiki wa kanisa hilo. Tayari hatua za awali zimeshaanza za kuchangisha michango mbalimbali kutoka kwaWakristo na pia kuna Harambee kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa inaandaliwa na inatarajiwa kufanyika
tarehe 29.04.2018 mara baada ya Ibada ya siku hiyo amabayo itakuwa moja na itaanza
saa 1:30 Asubuhi. Kama kanisa tunomba msaada kwa yoyote yule anayependa kusaidiana na Wakristo hawa katika kuitenda kazi ya Bwana. Kwa mwenye mchango tafadhali awasiliane na Mwenyekiti wa Harambee ya Upanuzi wa Kanisa
MR Pangisa kwa Simu Namba 0787449640. Mungu akubariki unapochangia kazi hii na kualika wengine katika kazi hii ya Mungu.
No comments:
Post a Comment